• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yasema askari watatu wa jeshi la DRC wauawa wakishambulia Rwanda, na DRC yaishutumu Rwanda kuvamia ardhi yake

    (GMT+08:00) 2018-02-16 17:09:04

    Jeshi la Rwanda limesema wanajeshi watatu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wameuawa kwenye mapambano baada ya kushambulia kituo cha jeshi la Rwanda kwenye wilaya ya Musanze kaskazini mashariki mwa Rwanda.

    Hatua hii imekuja siku chache baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kushutumu kuwa wanajeshi wa Rwanda wamevamia eneo la ardhi yake. Jumatano msemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alisema mapigano makali yalizuka kati ya jeshi la DRC na wapiganaji wa jeshi la Rwanda katika eneo la Mlima Nikone kwenye jimbo la Kivu Kaskazini, na kuripoti tukio hilo kwa kundi la nchi za maziwa makuu.

    Msemaji wa Divisheni ya pili ya jeshi la Rwanda Bw. Eugene Nkubito amesema majeshi ya DRC yalishambulia vikosi vyake katika kijiji cha Iterambere jumanne asubuhi lakini waliwaua wapiganaji watatu na kuwafukuza wengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako