• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Asali ya Tanzania yaweza kupata soko kubwa duniani

    (GMT+08:00) 2018-02-16 17:57:58

    Watanzania wamehimizwa kufuga nyuki kwa wingi ili kukuza uchumi kwa kutumia fursa ya upatikanaji wa asali na nta baada ya kuwapo kwa uhakika wa soko la nje kutokana na nchi zaidi ya 24 duniani kuagiza zao hilo.

    Tanzania inatajwa kuwa nchi ya pili duniani kwa uzalishaji wa asali ambapo huzalisha tani 38,000 kwa mwaka huku ikichuana na Ethiopia inayozalisha tani 50,000.

    Akizungumza katika ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) juzi, Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Glory Mziray alisema mahitaji ya asali duniani ni makubwa kuliko uzalishaji ulipo.

    Mziray alisema uzalishaji wa asali uko chini na kuwa, kwa sasa Tanzania inaweza kusafirisha asilimia 10 ya asali nje ya nchi huku asilimia 90 ikitumika nchini.

    Alizitaja nchi zinazohitaji zao hilo kwa wingi kuwa ni Afrika Kusini, India, Botswana, Namibia, Canada, Dubai, Kuwait, Irak, Iran, Japan, China na Lebanon.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako