• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajitahidi kuandaa vizuri michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi

    (GMT+08:00) 2018-02-21 17:45:48

    Michezo ya 23 ya Olimpiki ya majira ya baridi itafungwa tarehe 25 ya mwezi huu huko Pyeongchang nchini Korea ya Kusini. Ukiwa mwenyeji wa michezo hiyo ijayo ya 24 itakayofanyika mwaka 2022, mji wa Chongli unaharakisha maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo.

    Kwenye Uwanja wa Skii wa Bustani ya Miyuanyunding ya Chongli ya mji wa Zhangjiakou, mtaalamu wa kutengeneza barafu kutoka Marekani Bw. Tyson Goodrich anasema,

    "Wachezaji wa timu ya taifa la China ya skii wanafanya mazoezi hapa. Kazi yangu ni kutengeneza vizuri relitheluji kwa mujibu wa vigezo vya michezo ya Olimpiki."

    Baada ya kufungwa kwa michezo ya 23 ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Pyeongchang, maandalizi ya michezo hiyo ya 24 itakayofanyika mwaka 2022 nchini China yanaharakishwa. Naibu mkuu wa Bustani ya Miyuanyunding Bw. Shu Wen anasema,

    "Bado tuna muda wa miaka minne. Tulianza kupanga na kujenga uwanja na majumba kwa ajili ya michezo hiyo mwaka juzi, na kazi zote za ujenzi zitamalizika kabla ya mwaka 2020.

    Kutokana na michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, China imetoa wito wa "watu milioni 300 kushiriki kwenye michezo ya theluji na barafu". Kwa nyakati tofauti, idara kuu ya michezo ya China ilitoa mipango miwili ya kuendeleza michezo ya kwenye theluji na barafu, jambo ambalo limewahamasisha wachina wengi kushiriki kwenye michezo hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako