• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Shirikisho barani Afrika: Simba yafuzu raundi ya kwanza, kukutana na El-Masry 

    (GMT+08:00) 2018-02-22 09:44:14
    Wekundu wa msimbazi, Simba sports club imecheza mchezo wake wa marudiano wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao Gendermarie nchini Djibouti, simba ilikuwa ikihitaji sare tu ili kuweza kusonga mbele.

    Goli pekee la Emmanuel Okwi raia wa Uganda limeiwezesha timu hiyo kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambapo itakutana na El-Masry ya Misri.

    Katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, samba iliibuka na ushindi wa goli 4-0, hivyo mchezo wa juzi ilikuwa ikihitaji sare tu au kufungwa idadi ndogo ya magoli.

    Timu nyingine ya Afrika Mashariki AFC Leopards ya Kenya imeyaaga mashindano hayo baada ya kulazimishwa sare na FOSA Juniors ya Madagascar. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 wiki iliyopita katika mchezo uliopigwa nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako