• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mauzo ya bidhaa na vyakula katika msimu wa sikukuu nchini China yazidi dola bilioni 146 za kimarekani

    (GMT+08:00) 2018-02-22 18:13:32

    Takwimu mpya zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, katika siku saba za mapumziko za sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, mauzo ya bidhaa na vyakula nchini China yalifikia dola za kimarekani bilioni 146, ambalo ni ongezeko la asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Wakati huohuo, shughuli za utalii pia zimepamba moto.

    Takwimu zinaonesha kuwa, katika msimu wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, ongezeko la matumizi ya watu katika maeneo ya utamaduni na burudani lilikuwa kubwa kuliko manunuzi na vyakula. Fedha zilizotumiwa katika kutembelea bustani ziliongezeka kwa asilimia 50, huku matumizi katika kutazama filamu yakiongezeka kwa asilimia 60. Mwaka huu, katika siku saba za mapumziko, wachina zaidi ya milioni 100 walitazama filamu, na mauzo ya filamu katika muda huo yalizidi yuan bilioni tano. Licha ya kutembelea bustani na kutazama filamu, kutembelea majumba ya makumbusho, maduka ya vitabu, na kutazama maonesho pia ni chaguo la watu wengi.

    "Katika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, mbali na nguo na vyakula bora, tuna mahitaji ya utamaduni."

    Katika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi ya mwaka huu, baadhi ya watu walirudi nyumbani kukutana na watu wa familia zao, na wengine walifanya utalii. Takwimu zilizotolewa na idara ya utalii ya China zinaonesha kuwa, katika siku hizo za mapumziko, idadi ya watu waliofanya utalii ndani ya China ilifikia milioni 386, ambalo ni ongezeko la asilimia 12.1. Meneja wa Shirika la Utalii la Mamapunda Hua Bei amesema, mwaka huu kulikuwa na mabadiliko, badala ya watoto kurudi nyumbani kukutana na wazazi, wazazi walikwenda sehemu watoto wao wanapofanya kazi ili kusherehekea nao mwaka mpya. Anasema,

    "Watalii wanazingatia ubora wa hoteli, na wanapendelea hoteli za anasa haswa zile zenye huduma kwa watoto wachanga na chemchem ya maji moto. Aidha mwaka huu, gharama za kutalii katika sehemu maarufu ikiwemo miji ya Beijing, Shanghai na Guangzhou hazikuongezeka, hivyo miji hiyo imewavutia watalii wengi."

    Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka huu watalii wengi walichagua sehemu zenye hali nzuri ya hewa, haswa kisiwa cha Hainan, kilichoko kusini zaidi nchini China. Wakati huohuo, utalii katika sehemu zenye baridi zaidi pia unapendwa na baadhi ya watu, kwani wanaweza kutazama mandhari ya theluji na kuteleza katika barafu.

    Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka huu ndani ya China, sehemu za Guangdong, Sichuan, Hunan, Jiangsu na Henan zilitembelewa zaidi na watalii, na nje ya China, nchi za Asia ya Kusini Mashariki, Argentina na Mexico zilipendwa zaidi na watalii kutoka China. Meneja mkuu wa Shirikisho la Benki la China Bw. Chen Han amesema, mwaka huu manunulizi ya watalii wa China katika nchi za nje yamepungua, anasema,

    "Watu wanapenda zaidi kutumia pesa katika kujaribu utamaduni, vyakula na mandhari za nchi za nje. Na hayo ni mahitaji ya ngazi ya juu zaidi kuliko manunulizi ya bidhaa."

    Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka huu wastani wa matumizi ya watalii wa China katika nchi za nje ulikuwa yuan elfu sita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako