• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Syria na mjumbe maalumu wa Russia wajadili mapambano dhidi ya ugaidi

    (GMT+08:00) 2018-02-23 09:43:00

    Rais Bashar al-Assad wa Syria jana mjini Damascus amekutana na mjumbe maalumu wa rais wa Russia anayeshughulikia suala la Syria Bw Alexander Lavrentiev, na kujadiliana naye kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mapambano dhidi ya ugaidi.

    Viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha uratibu na ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi, na kujadili jinsi pande hizo mbili zitakavyofanya juhudi za pamoja kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Syria.

    Jumatano wiki hii, Balozi wa kudumu wa Russia kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Vassily Nebenzia alitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja huo kujadili hali ya eneo la mashariki mwa Damascus, na kusema madai yaliyotolewa na nchi za magharibi ya kusimamisha vita kwenye eneo la Guta mashariki, lililoko mashariki mwa mji wa Damascus, ni ya upande mmoja, na hayakuzingatia msimamo wa serikali ya Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako