• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania na Rwanda zaongoza katika vita dhidi ya ufisadi

    (GMT+08:00) 2018-02-23 17:31:08

    Tanzania imepanda kwa nafasi tatu katika vita dhidi ya rushwa kutoka nafasi ya 116 mwaka 2016 hadi nafasi ya 104 mwaka jana.

    Taarifa ya taasisi ya kimataifa ya Transparency International imeeleza kuwa, Tanzania imepata pointi 36 mwaka jana kutoka pointi 32 za mwaka juzi . Aidha nchi ya Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa Afrika Mashariki, ikiongozwa na Rwanda ambayo imeshika nafasi ya 48 kwa mwaka jana ikiwa na pointi 55. Hata hivyo, Rwanda imepanda kwa nafasi nne, kutoka nafasi ya 58 ikiwa na pointi 54 hadi nafasi ya 48.

    Kenya ilishika nafasi ya 143 wakati Uganda walishika nafasi ya 151. Hali hiyo imeifanya Kenya kuwa kwenye nafasi ya tatu Afrika Mashariki huku Uganda ikishika nafasi ya nne. Burundi imeshika nafasi ya 157 na Sudan Kusini nafasi ya 179 kati ya nchi 180.

    Burundi na Sudan Kusini zimetajwa kuwa kwenye nafasi mbaya kwenye ripoti hiyo ya dunia. Mkurugenzi Mtendaji wa Transparency International, Patricia Moreira alifafanua kuwa ripoti ya rushwa ya kimataifa kwa mwaka 2017, inaonesha kuwa nchi nyingi hazina maendeleo na mwelekeo mzuri wa kukomesha rushwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako