• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watalii zaidi wawasili kwa meli mjini Mombasa Kenya

    (GMT+08:00) 2018-02-23 17:31:45

    Zaidi ya watalii 1000 wamewasili kwa meli katika mji wa Mombasa nchini Kenya ikiwa ni ufanisi mkubwa katika sekta ya utalii kwenye msimu huu wa mwisho ambapo umepata ongezeko la asilimia 10.Afisa wa uhusiano mwema katika bandari ya Mombasa Bw Benard Osero amesema tangu mwaka jana kumekuwa na mafanikio makubwa sana kutokana na mikakati ifaayo iliyowekwa na serikali. Osero ameongeza kuwa hivi sasa Bandari ya Mombasa inalenga kupanua eneo la kutia nanga ili kuvutia watalii wengi wanaowasili kwa meli.Ameongeza kuwa wanalenga kupata watalii zaidi kutoka Miami Marekani na barani Ulaya.Mwaka 2016, serikali ilizindua ujenzi wa eneo la kutia nanga litakalojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 350.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako