• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bandari ya Dar es salaam kupanuliwa

    (GMT+08:00) 2018-02-23 17:32:05

    Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA) imesema kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam utawezesha mamlaka hiyo kuwa na uwezo wa kupokea meli yenye urefu wa mita 306 badala ya mita 245 zinazoingia sasa.

    Mradi huo wa Dar es Salaam Maritime Gateway Project (DMGP) umeanza kutekelezwa kwa kuboresha gati namba moja mpaka saba kwa thamani ya Sh bilioni 336 na unatarajiwa kukamilika Februari 2020.

    Mkurugenzi wa TPA, anayeshukughulikia Miundombinu, Karim Mattaka amesema mradi huo utafanya marekebisho katika gati namba moja mpaka namba saba ikiwa ni pamoja na kuongeza kina pamoja na miundombinu ya bandari ikiwa ni pamoja na kuboresha ulinzi.

    Amesema uingiaji wa meli zenye urefu mkubwa katika bandari hiyo ni mgumu kwa kuwa haina uwezo wa kupokea meli hizo kutokana na mita za urefu katika eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako