• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapigano yaendelea mjini Ghouta nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-02-23 18:24:53

    Mashambulizi ya anga yameendelea jana katika eneo la mwisho lililozingirwa na waasi katika mji mkuu wa Syria wakati huu ambapo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeagiza kupatikana suluhu, na likiwa limeitisha siku thelathini za kusimamisha mapigano katika nchi hiyo.

    Wakati huohuo, majeshi ya serikali ya Syria limewataka raia waliosalia katika mji Ghouta ulioko mashariki ya Damascus kusogea katika maeneo linayoyashikilia, na limewapa maelekezo ya jinsi ya kutoka salama kwa kutumia vipeperushi vilivyosambazwa kwa njia ya helikopta.

    Alhamisi iliyopita baraza la usalama lilifanya mkutano wa kujadili mapigano yanayoendelea katika eneo la Ghouta, lakini likishindwa kufanya makubaliano ya jinsi ya kisitisha mapigano.

    Ripoti kuhusu vifo vya raia na mashambulizi katika hospital kutokana na mapigano makali yaliyozuka hivi karibuni mjini Ghouta zimepekelea pande mbalimbali duniani kutoa wito wa kusitisha mapigano.

    Shambulizi lililofanywa mjini Ghouta eneo ambalo linashikiliwa na waasi, linaaminika kuwa la kutisha zaidi katika kipindi cha miaka saba ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako