• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa kusimamisha mapigano Syria

    (GMT+08:00) 2018-02-23 19:19:17

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jana ametoa wito wa kusimamisha mara moja mapigano katika eneo linalokaliwa na waasi la Ghouta Mashariki nchini Syria.

    Bw. Guterres amesema hayo kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambapo ameeleza kusikitishwa kwake na mateso makali wanayopata raia wanaoishi kwenye eneo hilo. Amezitaka pande zinazopingana kwenye eneo hilo kusimamisha mapigano na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wahitaji na kuruhusu kuondolewa kwa watu 700 wanaohitaji matibabu ya haraka ambayo hayaweze kupatikana katika eneo hilo.

    Wakati huohuo, Bw. Guterres amerejea tena umuhimu wa mitazamo ya kivitendo katika kuzuia badala ya kukabiliana na migogoro. Amesema kuzuia migogoro ni wajibu wa msingi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, na kwamba Umoja huo uko tayari kusaidia nchi hizo kutatua migogoro yao na kuzuia kutokea kwa machafuko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako