• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupiga kura ya maoni kuhusu azimio la kusimamisha vita nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-02-23 20:22:36

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo saa 5 kwa saa za mashariki ya Marekani litafanya zoezi la upigaji kura za maoni kuhusu muswada wa azimio la kusimamisha vita kwa siku 30 nchini Syria.

    Jana alasiri baraza hilo lilifanya mkutano na kujadili hali ya Syria. Kutokana na tofauti ya maoni ya nchi wanachama, baraza la usalama halikufanya upigaji kura kuhusu azimio hilo lililotolewa na wajumbe wa kudumu ambao ni Sweden na Kuwait kwenye Umoja wa Mataifa.

    Habari zilisema kuwa muswada huo ulizitaka pande husika zisimamishe vita, ziondoke katika maeneo manne zinayoyazunguka ya huko Damascus, kuhakikisha njia ya usafirishaji ili kuhakikisha usalama wakati wa utoaji wa vyakula na madawa kwa wenyeji wanaoishi kwenye maeneo hayo. Lakini muswada huo sio pamoja na zile operesheni za kupambana na kundi la IS na kundi la Qaeda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako