• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya, Uganda wazindua kituo cha forodha

    (GMT+08:00) 2018-02-26 20:26:31

    RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta na mshirika wake Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, wamesaini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika maeneo ya mipaka yanayounganisha nchi hizo mbili.

    Viongozi hao wakiwa katika eneo la Busia, wamezindua kituo cha Forodha kitakachotumiwa kwa pamoja na nchi zote mbili (OSBP) chenye thamani ya Sh bilioni 1.2, kilichojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza.

    Katika mazungumzo yao, pamoja na kukubaliana kuongeza ushirikiano zaidi kwenye maeneo ya mipaka kwa kufungua fursa kwa nchi zote mbili, walionesha wasiwasi kuhusu kutumika vibaya kwa mipaka hiyo na wahamiaji haramu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako