• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kampuni ya nguo imesema mishahara na ada za juu umeme imesukuma gharama ya uzalishaji

    (GMT+08:00) 2018-02-26 20:30:21

    Kampuni ya nguo ya Dubai inayofanya kazi nchini Kenya imesema kuwa gharama kubwa ya umeme na mapato ya kiwango cha chini imesukuma juu gharama za uzalishaji.

    United Aryan (EPZ) Ltd, imefanyakazi nchini Kenya kwa kipindi cha miaka 16 iliyopita, na imesema bado inalipa ada kubwa ya nishati na matumizi makubwa kwa mishahara ikilinganishwa na nchi kama vile Ethiopia, Rwanda, Malawi na Misri ambapo gharama za kazi ni nafuu.

    Mshahara wa chini nchini Kenya sasa ni sh13,475na, inatarajiwa kuongezeka hadi

    Sh15, 372 mwaka huu ikiwa mapendekezo ya chama cha wafanyikazi cha COTU litathibitishwa.

    Sekta ya viwanda nchini Kenya ina uwezo mkubwa sana wa ukuaji tofauti na nchi nyingine katika mkoa wa Afrika Mashariki.

    Ada za juu za umeme zimesababisha bidhaa za Kenya kukosa soko.

    Uagizaji wa bidhaa za bei nafuu kutoka kwa masoko ya kimataifa na ya kikanda, na kunyima mapato ya viwanda vya ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako