• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kampuni ya umeme ya Kenya Power, imeandikisha kushuka kwa asimilia 30.3 ya faida baada ya kodi

    (GMT+08:00) 2018-02-26 20:31:04

    Kampuni ya umeme ya Kenya Power, imeandikisha kushuka kwa asimilia 30.3 ya faida baada ya kodi na kufikia sh bilioni 2.97 ikilinganishwa na sh bilioni 4.2 iliyoandikishwa wakati huo huo mwaka 2016.

    Taarifa kutoka kwa wasambazaji wa nguvu za umeme ni kwamba kushuka kwa faida kumesababishwa kushuka kwa uchumi na ongezeko la gharama ya fedha.

    Mauzo ya umeme iliongezeka kwa asilimia 2.3 kutoka gigawati 3,805 mwaka 2016 hadi gigawati 3,893.

    Kutokana na kuongezeka kwa mauzo mapato ya mauzo iliongezeka hadi Sh bilioni 46.93 kutoka Sh bilioni 45.79 mwaka 2016.

    Upungufu wa faida unakuja wakati Wakenya wanalalamika kwa bei kubwa za umeme.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako