• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la Dunia: Rais Kenyatta apokea msafara wa ziara ya dunia ya tuzo ya mabingwa wa kombe la dunia mwaka huu

  (GMT+08:00) 2018-02-27 10:00:09

  Rais Uhuru Kenyatta jana aliipokea tuzo ya washindi wa kombe la dunia na kuwakaribisha wajumbe wa msafara wa ziara ya dunia ya kombe hilo ambao waliwasili nchini Kenya wakitokea nchini Ethiopia.

  Katika hotuba yake ya kupokea kombe hilo aliyoitoa akiwa ikulu jijini Nairobi, alilishukuru shirikisho la mpira wa miguu la dunia FIFA, na aliahidi kuwa serikali yake itajitahidi kuendeleza mchezo huo nchini Kenya.

  Kombe hilo ambalo ni wakuu wa nchi pekee wanaoruhusiwa kuligusa, leo jumanne litawekwa katika eneo la wazi kwenye ukumbi wa mikutano wa KICC jijini Nairobi ili raia wa Kenya wapate fursa kuliona, na kesho jumatano msafara utaondoka kuelekea nchini Msumbiji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako