• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa Leba Kenya,Ukur Yattani avitaka vyama vya wafanyakazi kusitisha migomo kwa kuwa inalemaza uchumi wa nchi

    (GMT+08:00) 2018-02-27 19:04:11

    Waziri wa Leba nchini Kenya Bw Ukur Yattani amevitaka vyama vya maslahi ya wafanyakazi kusitisha hatua ya kugoma.

    Wiki iliyopita chama cha wafanyakazi wa vyuo vikuu (Kusu) pamoja na Chama cha Wahadhiri (Uasu) vilitoa ilani ya siku saba ya kabla ya kuanza mgomo kutokana na kile wanachodai ni kuwa serikali imekataa kuwasilisha mapendekezo ya nyongeza ya mishahara.

    Waziri Yattani alizungumza jana jijini Nairobi na kuvishauri vyama hivyo kufanya mazungumzo na serikali.

    Aidha Yattani alisema migomo ya mara kwa mara inalemaza uchumi wa nchi.

    Wakati huo huo Waziri Yattani alisema atakutana na vingozi wa vyama vya wafanyakazi ili kusikiliza malalmishi yao.

    Mwaka jana kulishuhudiwa migomo ya wafanyakazi wengi wa umma kama vile madaktari,wahadhiri,manesi,wafanyakazi wa vyuo vikuu na walimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako