• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya kuzalisha mahindi zaidi

    (GMT+08:00) 2018-02-27 19:04:36

    Serikali ya Kenya inalenga kuzalisha magunia milioni 2.8 ya mahindi mwaka huu ili kukabiliana na uhaba wa chakula.

    Kupitia wizara ya Kilimo,serikali inalenga kuongeza ardhi itakayotumia kwa shughuli za kilimo kwa ekari 52,000.

    Naibu Mkurugenzi katika idara ya Kilimo Bi Grace Chirchir amesema serikali pia inalenga kuongeza kiasi hicho kwa ekari 70,000 zaidi kupitia mpango wa kuwashirikisha wakulima binafsi.

    Alisema wanalenga kushirikisha wakulima 20,000 ambao watanufaika kwa huduma mbalimbali za kilimo ambazo zitatolewa bila malipo yoyote.

    Aidha alisema serikali imejitolea kuhakikisha kwamba inaimraisha sekta ya kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako