• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Mauzo ya kahawa ya Rwanda yaongezeka

    (GMT+08:00) 2018-02-28 19:18:06

    Mauzo ya kila mwaka ya kahawa ya Rwanda yameongezeka na kuiletea nchi hiyo dola milioni 64 mwaka wa 2017.

    Ripoti ya halmashauri ya kuuza nje bidhaa za kilimo inasema mapato ya mwaka 2016 yalikuwa dola milioni 58.5.

    Halmashsuri hiyo imesema kuongezeka kwa mapato kumechangiwa na kuimarika kwa bei katika soko la kimataifa ambayo ilifikia dola 3.7 kwa kilo hadi desemba mwaka 2017.

    Aidha Rwanda iliuza zaidi ya kilo milioni 1.8 wakati huo ikilinganishwa na kilo milioni 1.4 za mwaka 2016.

    Kahawa ndio zao kuu ambayo Rwanda inauza kwenye masoko ya nje ikiwakilisha asilimia 24 ya mauzo yote ya bidhaa za kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako