• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Shoprite kufungua matawi Kenya

    (GMT+08:00) 2018-02-28 19:20:08

    Kampuni ya maduka makubwa ya rejareja ya Afrika Kusini Shoprite, imepata nafasi ya kufungua matawi katika maeneo saba nchini Kenya na inatarajia kuanza biashara ndani ya miezi kadhaa ijayo.

    Mkurugenzi wa maduka hayo Pieter Engelbrecht, amesema tayari wamesaini makubaliano na wenye majumba ambako matawi hayo yatafunguliwa.

    Engelbrecht amesema upanuzi unaendelea barani Afrika na mwaka 2017 walifungua matawi 150 katika nchi 14 na hivyo kufungua nafasi 4,254 za ajira.

    Hadi sasa Shoprite ina maduka 2,811 na waajiri 148,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako