• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali yakutana na wadau wa maendeleo

    (GMT+08:00) 2018-02-28 19:20:46

    Serikali ya Tanzania imeanza mazungumzo na Kundi la Wadau wa Maendeleo (DPG) ili kuondoa tofauti zilizojitokeza baina yao na kusababisha baadhi ya wadau hao, kutotoa fedha kuchangia miradi ya maendeleo nchini.

    Akifungua Mkutano wa Majadiliano ya kimkakati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, mjini Dodoma jana, amesema mkutano huo wa siku mbili, ni wa kwanza kufanyika na unalenga kurudisha uhusiano mzuri uliokuwapo awali kati ya serikali na wadau hao wa maendeleo.

    James amesema mkutano mwingine wa kukamilisha mazungumzo utafanyika Novemba mwaka huu, lengo ni kuhakikisha uhusiano mzuri uliokuwa awali, ambao ulilega lega miaka ya karibuni, unarudi na kuimarika na kuwa mzuri zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako