• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar yaomba huduma za ATCL zifike Pemba

    (GMT+08:00) 2018-02-28 19:21:06

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imeanza mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kuhusu uwezekano wa kutoa huduma za safari za anga katika kisiwa cha Pemba.

    Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mohamed Ahmada wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Chakechake, Suleiman Sarhani aliyetaka kujua kwa nini hadi sasa ATCL ambayo ni taasisi ya muungano imeshindwa kufanya safari zake katika kisiwa cha Pemba na kulipatia ufumbuzi tatizo la usafiri linalowakabili wananchi.

    Alisema ni kweli huduma nyingi zimeimarika katika kisiwa cha Pemba ikiwemo sekta ya utalii na biashara ambapo suala la kuwepo kwa huduma za ndege za uhakika zinahitajika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako