• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Mgao wa maji kuendelea kwa miaka 4 ijayo

    (GMT+08:00) 2018-03-01 19:24:04

    Wakaazi takriban milioni 4 wanaoishi katika kaunti ya Nairobi wataendelea kupokea maji kwa mgao hadi mwaka 2023.

    Hili limethibitishwa na kampuni ya Maji kupitia kwa mhandisi Nahashon Muguna anayesema viwango vya maji katika dimbwi la Ndakaini vimeshukwa kwa asilimia 49.

    Kwa maelezo yake kwa vyombo vya habari maji yamefikia cubic mita milioni 34 na hayatoshi kutimiza mahitaji ya idadi ya watu Nairobi.

    Bodi ya maji aidha imeahidi kuendelea kusambaza maji ya cubic mita 525,000 kila siku ili kuwawezesha wakazi kutumia maji kwa matumizi ya msingi.

    Serikali kuu pamoja na serikali ya kaunti zimekubali kubuni mbinu mbada ya kupata maji ya kutosha

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako