• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Oparesheni ya ukaguzi wa vituo vya kubadilisha fedha kuendelea Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-03-01 19:24:24

    Benki kuu ya Tanzania imesisitiza kuendeleza msako wa kukagua na kufunga vituo vya kubadilisha fedha vinavyotoa huduma kinyume na sheria.

    Kufikia mwezi wa Februari,zaidi ya vituo 110 vya huduma za fedha pamoja na benki 5 za biashara zilifungwa baada ya kupatikana na hatia hiyo.

    Eliamringi Mandari mkurugeni wa benki kuu ya Tanzania amesema vituo 71 vimefanyiwa uchunguzi na kushurutishwa kusajiliwa upya ili wapate leseni za kuendesha biashara hiyo.

    Kwa mujibu wa sehria za huduma za fedha vituo hivyo vinatakiwa kuwa na mtaji wa shilingi milioni 100 za Tanzania .

    Thuluthi mbili ya fedha hizo zinapaswa kuwa taslimu kwa ajili ya harakati za kila siku.

    Katika jumla ya vituo 297 vya kubadilisha fedha nchini Tanzania vituo kadhaa vya Daresalaam,Arusha na Kilimanjaro vimepokonywa leseni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako