• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Serikali kukabiliana na ukame

    (GMT+08:00) 2018-03-01 19:24:58

    Serikali imetangaza hatua za kukabiliana na athari za kipindi kirefu cha kiangazi ambacho kimekumba maeneo mbalimbali nchini.

    Msemaji wa wa polisi Eric Kiraithe anasema baadhi ya mipango hiyo ni utekelezaji wa Mradi wa Kitaifa wa Maji.

    Hatua hiyo itahakikisha kukamilishwa kwa mabwawa kadhaa yanayojengwa nchini ili kukusanya maji ya kutumika wakati wa kiangazi.

    Serikali imesema kwamba inashirikiana na mashirika husika kuhakikisha kiangazi kinachojiri nchini kimedhibitiwa.

    Wakati huo huo, serikali ya kitaifa imesema kuwa itaanza kusambaza maji kwa maeneo ya wafugaji wa kuhamahama ili kushughulikia upungufu wa bidhaa hiyo. Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa anasema kuna mikakati ya kuhakikisha wananchi hawafariki kutokana na njaa huku ikiwa tayari imeanza kusambaza chakula cha msaada katika kaunti 14 ambazo zimeathirika zaidi na baa la njaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako