• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Laini za simu Tanzania zafika zaidi ya milioni 40

  (GMT+08:00) 2018-03-02 19:41:23

  Laini za simu za mikononi nchini Tanzania zimeongezeka kutoka 2,198 mwaka 1995 hadi kufikia zaidi ya milioni 40 ilipofi ka Desemba mwaka jana, ambazo zipo mikononi mwa watu na hivyo kuendeleza ustawi wa Watanzania.

  Wakati huo huo, serikali pia imezindua mfumo wa kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole (biometria), ambao utadhibiti changamoto za usajili zilizopo. Changamoto hizo ni pamoja na udanganyifu unaofanyika sasa kwa kutumia laini za sasa, sambamba na kuisaidia serikali kuwa na takwimu sahihi ya watumiaji wa huduma za simu za mkononi, zitakazosaidia kuweka mipango ya uchumi wa Taifa.

  Mwakilishi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kitolina Kippa amesema ongezeko hilo kubwa na la haraka la laini za simu, limekuja baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa utoaji wa leseni unaozingatia mwingiliano wa teknolojia mwaka 2005. Akizungumzia usajili wa laini za simu kwa kidole, Kippa amesema utafanyika kwa majaribio katika mikoa sita nchini. Alisema pamoja na kuwepo matumizi sahihi ya simu za mkononi, bado kuna watumiaji wachache ambao wanatumia huduma za mawasiliano vibaya. Alisema mfumo huo wa usajili ni hatua muhimu ya matumizi ya teknolojia katika kudhibiti changamoto za usajili na kuwezesha watoa huduma, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na serikali kuwa na takwimu sahihi za watumiaji wa huduma za simu za mkononi na vifaa vingine vya mawasiliano vinavyotumia laini za simu. Pia alisema kuwepo kumbukumbu sahihi za laini za simu, kutafanikisha kuanzishwa na kuwekwa kwa Data ya laini za simu zilizosajiliwa ambayo inatakiwa na TCRA.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako