• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yahakikishia wenye viwanda nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-03-02 19:46:04

    Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Tanzania Jumaa Aweso amewahakikishia wenye viwanda kuwa wizara yake itatumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda hivyo katika miradi yake ya maji.

    Aweso aliyasema hayo wakati alipotembelea kiwanda cha Plasco kinachozalisha mabomba ya usambazaji maji kilichopo eneo la Chang'ombe Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

    Amewashauri Watanzania kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya nyumbani kwa kuwa nyingi zina ubora na pia kusaidia serikali kukusanya pato huku manunuzi yao yakisaidia kuwapatia vijana ajira na kukuza uchumi.

    Aidha amewataka wamiliki wa kiwanda hicho kuendelea kuzingatia ubora na viwango katika bidhaa wanazozalisha ili ziendane na huduma na kuwahakikishia kuwa wizara yake haitakuwa na kikwazo kwa viwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako