• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Telkom kupata mkopo wa sh bilioni 4 kuboresha huduma za mtandao

    (GMT+08:00) 2018-03-05 19:18:39

    Kampuni ya mawasiliano Telkom Kenya imejipanga kupokea mkopo wa dola miloni 40 sawa na sh bilioni 4.1 kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya ili kuongeza miundo msingi na huduma za fedha za simu hiyo.

    Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) imesema mkopo, ambao bado unaendelea kupitia tathmini, itafadhili tu, mradi wa upanuzi wa huduma za mtandao ambayo inatarajiwa kugharimu sh bilioni 9.34

    Telkom Kenya imesema kuwa mkakati wake wa miaka mitano ni kuwekeza jumla ya Sh bilioni 15.2 bilioni, ($150 million) katika mitandao yake ya 3G na 4G pamoja na huduma za fedha za simu na uzoefu wa wateja.

    Aidha amesema tayari imewekeza karibu Sh bilioni 5.6 katika kupanua na kuboresha mtandao wake, ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa huduma za 4G.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako