• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Ujenzi wa reli ya juu ya kisasa Dar wazinduliwa

    (GMT+08:00) 2018-03-05 19:19:15
    WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa amezindua ujenzi wa reli ya juu ya kisasa (SGR) yenye kilometa mbili itakayojengwa Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia Stesheni hadi Buguruni.
    Aidha amesema reli hiyo ya kati inalenga kuwezesha treni kuendelea na safari yake bila kusababisha msongamano wa magari.
    ujenzi wa reli ya kati utarajiwa kukamilika ifikapo Julai mwaka 2019.
    Alisisitiza kuwa miradi hiyo itagharimu Sh trilioni 7.6, na wanatarajia ifikapo mwaka 2020 treni ya kisasa itazinduliwa.
    mradi unaangaliwa kuleta maendeleo kwa taifa kwani ni fedha za kodi za wananchi zinatumika.
    Pia alieleza kuwa serikali imefanya uwekezaji mkubwa ambao ni lazima waone matunda ya mradi huo kwa malengo ya kuongeza pato la Taifa.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako