• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: China kuongeza kampeni ya watalii wake kwenda Rwanda

  (GMT+08:00) 2018-03-06 19:59:25

  Mkurungezi wa utalii katika manispaa ya Guangzhou nchini China Liu Yumei ameahidi kufanya kazi kwa pamoja na maafisa wa Rwanda ili kuongeza idadi ya watalii wa China kwenda Rwanda.

  Yumei aliyasema hayo wakati wa kufungwa kwa maonyesho ya usafiri ya siku tatu ya kiataifa mjini Guangzhou.

  Alisema manispaa hiyo ina uhusiano wa muda mrefu na Rwanda na hasa katika sekta ya utalii na watarajia kushirikiana kuendeleza sekta hiyo.

  Maonyesho hayo yaliwaleta pamoja taasisi za serikali na mashirika ya usafiri na utalii kote duniani.

  Naye mwakilishi wa shirika la ndege la Rwanda RwandAir mjini Guanzhou Paul Guo alisema safari za kati ya Kigali na Guangzhou zinazotarajiwa kuanza mwezi Juni zitasaidia kukuza biashar, uwekezaji na utalii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako