• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya yapiga marufuku nyama kutoka Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-03-07 20:10:02

    Kenya imepiga marufuku uagiziaji na uuzaji wa nyama kutoka Afrika Kusini kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa listeriosis wiki iliopita.

    Mkurungezi wa afya ya umma bwana Kepha Ombacho, amewataka maafisa wote wa afya kwenye maeneo ya mipakani kutekeleza marufuku hiyo hasa kwa nyama za makampuni ya Enterprise Food Production Factory na Rainbow Chicken Limited.

    Ombacho amesema idara ya afya ya umma inashirikiana na maafisa wote wa afya kote nchini humo ili kuhakikisha hakuna bidhaa zilizo chini ya marufuku zinaingia nchini.

    Baadhi ya maduka makubwa kama vile Tuskys, Naivas na Carrefour kwa sasa hayana bidhaa za nyama kutoka Afrika Kusini.

    Meneja wa duka la Carrefour Franck Moreau amesema hawana ushirikian wa kibiashara na kampuni hizo mbili za Afrika Kusini, na kwamba bidhaa zao nyingi za nyama hununuliwa Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako