• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: EABL yahitaji baa 4,000 kuuza bidhaa zake za kiwanda kipya kisumu

    (GMT+08:00) 2018-03-07 20:10:22

    Kampuni ya mvinyo East Africa Breweries (EABL) imesema itahitaji baa 4,000 mpya ili kuuza kikamilifu pombe itakayotengenezwa kwenye kiwanda chake kipya mjini Kisimu, Magharibi mwa Kenya.

    Kampuni hiyo pia imesema kiwanda hicho ambacho kitakamilika Julai mwaka ujao kitaajiri wasambazaji 12 kwenye eneo hilo.

    Aidha kiwanda hicho kipya kitaajiri moja kwa moja watu 100 na kuongeza idadi ya wakulima wa mawele kufikia 30,000.

    EABL ambayo hisa zake nyingi zinamilikiwa na kampuni ya Uingereza ya Diageo, kwa sasa inauza bidhaa zake kwa zaidi ya baa 20 kote nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako