• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Bei ya mafuta yaongezeka

    (GMT+08:00) 2018-03-07 20:10:43

    Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewuara) imetangaza bei kikomo za mafuta kwa mwezi huu huku bei ya petrol na dizeli ikiongezeka.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura,Nzinyangwa Mchany,katika bei hizo zinazoanza kutumika leo,bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote yaliyoingizwa nchini Tanzania kupitia bandari ya Dar es Salaam,zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la Februari 7.

    Mchany alisema kuwa kwa mwezi huu,bei za rejareja za petroli zimeongezeka kwa Sh.1 kwa lita (ongezeko la asilimia 0.06) ,dizeli Sh.69 kwa lita (asilimia 3.37) ,na mafuta ya taa Sh.4 kwa lita (ongezeko la asilimia 0.20).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako