• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wafanya biashara wa Ufaransa wasaka fursa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-03-07 20:11:00

    Ujumbe wa wafanyabiashara 40 kutoka Ufaransa unatarajiwa kuwasili mwezi ujao kwa ajili ya kuona fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.

    Hayo yamebainishwa jana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier alipotembelea ofisi za kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) ambayo huchapisha magazeti ya 'Habari Leo', 'Daily News' na 'SpotiLeo'.

    Balozi Clavier amesifu juhudi zinazofanywa na magazeti hayo kwa jili ya kuelimisha wananchi pamoja na juhudi ya kueleza fursa mbalimbali zilizopo nchini kupitia Jukwaa la Biashara linaloandaliwa na TSN ambalo litafanyika Zanzibar Machi 15, mwaka huu. Kutokana na uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili, mwanadiplomasia huyo amewakaribisha Wafanyabiashara wa Tanzania kwenda kuwekeza nchini Ufaransa.

    Pia, Balozi Clavier ameahidi kuboresha mahusiano baina ya waandishi wa habari wa TSN na waandishi wa habari wa Ufaransa kubadilishana ujuzi na uzoefu ikiwa ni jitihada za kuendeleza mahusinao ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako