• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Utafutaji mafuta waaanza ziwa Kivu

  (GMT+08:00) 2018-03-07 20:11:23

  Kampuni moja ya Rwanda-Ngali Mining ambayo ilishinda haki za kufanya utafutaji katika ziwa la Kivu imetoa kandarasi kwa kampuni ya Uingereza kutafuta mafuta eneo hilo.

  Kampuni hiyo ya Uingereza ABI Holdings itafanya utafutaji kwenye kanda ya mashariki ya ziwa Kivu.

  Mwaka wa 2014 ilibainika kuwa kuna uwezekano wa kuwa na mafuta lakini utafutaji ulisimamishwa baada ya serikali kukosa kukubaliana kuhusu haki kati yake na makampuni ya kigeni.

  Mkuu wa halmashauri ya petrol na gesi nchini humo Francis Gatare, amethibitisha kuwa utafutaji wa mafuta unaendelea lakini hajataja utaendelea kwa muda gani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako