• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Wizara ya fedha kudhibiti IFMIS ili kupunguza ubadhirifu wa fedha

  (GMT+08:00) 2018-03-08 18:56:23

  Wizara ya fedha nchini Kenya itadhibiti mfumo wa usimamzi wa fedha (Ifmis) unaodaiwa kutumiwa vibaya katika ubadhirifu wa fedha za serikali.

  Mfumo huo wa Ifmis ulibuniwa na serikali ili kuzuia uporaji na ufisadi kwa mujinu wa mkaguzi mkuu Edward Ouko.

  Kwa sasa mpango mpya wa kudhibiti mfumo huo utatumika ikiwa ni pamoja na kuweko kwa vifaa vya kuzuia udanganyifu .

  Mbali na haya,Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa ajenda yake yenye maswala manne makuu inatoa fursa nyingi kwa sekta ya kibinafsi kuleta utajiri kwa raia wa nchi hii.

  Amesema kuwa ajenda hiyo inayoangazia utengenenzaji bidhaa, huduma za afya kwa wote, makazi ya bei nafuu na chakula cha kutosha inalenga kuimarisha ustawi wa nchi hii, kuleta utajiri na kubuni nafasi za ajira kwa vijana.

  Katika muda wa miaka mitano ijayo serikali inanuia kuimarisha utengenezaji bidhaa na kuzidisha mchango wake kwa pato jumla la kitaifa kutoka asilimia 9 hadi asilimia 15, kuhakikisha huduma za afya kwa wote, kufanikisha ujenzi wa nyumba nusu milioni za gharama nafuu na kuhakikisha kuna chakula cha kutosha

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako