• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania;Zanzibar kutengeza simu

  (GMT+08:00) 2018-03-08 18:56:42

  Zanzibar inatarajia kujenga kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza simu za mkononi na kutoa ajira kwa wananchi wa visiwa hivyo.

  Kiwanda hicho kitakachoanzishwa hivi karibuni na Kampuni ya U$I kutoka Korea Kusini, kitaanza kwa kuunganisha vifaa vya simu na kisha baada ya miaka minne kuanza kutengeneza simu.

  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud alisema kwa sasa wanaanzisha viwanda vikubwa vyenye kukuza uzalishaji, kuleta ajira na kukuza pato la taifa.

  Alisema wiki mbili zilizopita, wamesaini makubaliano na kiwanda cha simu za mkononi na tayari wawekezaji hao wamepewa eneo katika eneo la viwanda vidogo. "Kwa sasa wanamalizia taratibu na wamesema katika miezi miwili hadi mitatu watakuwa wameanza kazi ya kuunganisha simu kutoka Korea Kusini, badala ya kununua kutoka Korea sasa zitakamilika hapa na kwenda kuuzwa maeneo mengine," alisema.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako