• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wafungwa zaidi ya elfu 30 wamepata msamaha katika miaka mitano nchini China

  (GMT+08:00) 2018-03-09 16:19:36

  Ripoti ya kazi za Mahakama Kuu ya China imeonyesha kuwa, jumla ya wafungwa 31,527 wamepewa msamaha nchini China katika miaka mitano iliyopita.

  Jaji mkuu wa China Zhou Qiang amesema hayo alipowasilisha ripoti ya kazi za mahakama katika kikao cha mkutano unaoendelea wa Bunge la Umma la China. Amesema mahakama nchini China zimeimarisha juhudi za kulinda haki za binadamu katika shughuli zake, na kwamba hukumu za kifo zinafanyiwa tathmini ya kina ili kuhakikisha kuwa hukumu hiyo inatolewa tu kwa idadi ndogo ya wahalifu kwa makosa makubwa sana.

  Ripoti hiyo imesema kesi zinazohusu watoto zimepungua kwa miaka mitano mfululizo, na kwamba Mahakama hiyo imeshirikiana na Wizara ya Sheria kuboresha mfumo wa msaada wa kisheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako