• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yafanya makubaliano na UNIDO ya kufikia uchumi wa kati

    (GMT+08:00) 2018-03-09 19:32:05

    Serikali ya Tanzania imesaini makubaliano na Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Viwanda (UNIDO) ya kuitoa Tanzania katika mipango ya kitaifa kwenda kwenye mipango ya nchi na washirika ili kufikia uchumi wa kati.

    Makubaliano hayo yalisainiwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO, Li yong. Mwijage amesema "UNIDO itaisaidia Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia uchumi wa viwanda. Amesema mambo ambayo wanatarajia kufanya kupitia makubaliano hayo ni UNIDO itakuwa na jukumu la kutafuta washirika wengine, kuja kuangalia namna gani wanaweza kusaidia katika mpango wa Taifa wa miaka mitano, ambao kwa sasa dhima yake ni ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kufanya mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Mwijage ameongeza kuwa mambo wanayotegemea kufanywa katika mpango miaka mitano ni kuendelea kujenga maeneo yaliyo rasmi ya uwekezaji, miundombinu wezeshi na saidizi. Amesema wamelenga kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla, huku malengo makuu matatu yakiwa ni kutengeneza ajira, kuzalisha bidhaa zenye viwango vya ubora wa hali ya juu na kuwapatia watu kipato kuanzia wanaoshiriki shambani hadi viwandani.Kwa upande wake, Yong amesema kuwa wataisaidia Tanzania katika mpango wa miaka mitano, ikiwemo kukuza sekta ya viwanda, ajira kwa wanawake na vijana na utunzaji wa mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako