• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yatakiwa kuweka sera za kuimarisha sekta ya uzalishaji umeme

  (GMT+08:00) 2018-03-09 19:32:24

  Serikali ya Kenya imeombwa kuweka sera bora zaidi zitakazoimarisha sekta ya uzalishaji umeme wa miale ya jua. Kampuni ya M-KOPA solar inayojihusisha na usambazaji wa vifaa vya kieletroniki vinavyotumia sola kwa bei nafuu imesema ingawa kuna mikakati ambayo tayari imewekwa na serikali kusaidia sekta hiyo, kuna mengi zaidi ambayo yanahitaji kufanywa. Mwenyekiti wa kampuni hiyo Mugo Kibati amesema kukiwa na sera mwafaka kama vile upunguzaji wa ushuru kwa watengenezaji wa sehemu zinazotumiwa kuunda vifaa vya sola, bei ya vifaa hivyo itapungua na itakuwa afueni kwa wananchi wenye mapato ya chini.Katika mpango wa serikali wa kusambaza umeme mashinani wananchi wenye mapato ya chini huunganishiwa umeme lakini bado wanahitajika kulipia ada za umeme.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako