• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viongozi wataka wanawake wawezeshwe kiuchumi

  (GMT+08:00) 2018-03-09 19:32:42

  Viongozi mbalimbali akiwemo Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli wametoa mwito kwa mashirika ya umma, sekta binafsi, asasi za kiraia na watu binafsi, kushirikiana na serikali katika kuwawezesha wanawake kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za mafunzo, mitaji na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.

  Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Mama Janeth amesema serikali imejitahidi kuweka usawa wa jinsia na kuwezesha wanawake kisiasa, kiuchumi, elimu na afya, lakini serikali pekee haiwezi kumaliza changamoto zote, hivyo ni lazima wananchi wenyewe washiriki. Aidha amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ambayo ni 'Kuelekea Uchumi wa Viwanda Tuimarishe Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini', imeendana na nia ya dhati ya serikali ya kujenga Tanzania ya viwanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako