• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wan Gang asema ushirikiano wa uvumbuzi wa sanyansi na teknolojia kati ya China na Marekani hauna kizuizi

  (GMT+08:00) 2018-03-10 17:32:25

  Waziri wa sayansi na teknolojia wa China Bw. Wan Gang hapa Beijing amesema, anawakaribisha wafanyabiashara wa Marekani kuja China, na kuzungumzia mambo mengi licha ya magari ya nishati ya umeme. Kama pande mbili zikiweza kufanya mawasiliano mengi zaidi, ushirikiano wa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia kati ya China na Marekani hautakabiliana na kizuzi.

  Bw. Wan amesema hayo kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika katika kituo cha habari cha mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China. Pia amesema, China na Marekani zinashirikiana vizuri kwenye sekta ya magari yanayotumia nishati ya umeme, wizara mbili za nishati za China na Marekani i zina kituo cha utafiti cha pamoja, ambacho kinafanya utaifiti wa pamoja kuhusu ujenzi wa majengo yanayobana matumizi ya nishati, matumizi ya makaa ya mawe kwa njia isiyoleta uchafuzi pamoja na magari ya umeme.

  Ameongeza kuwa nchi hizo mbili hazina kizuizi katika ushirikiano wa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia. Tatizo lolote litaweza kutatuliwa kwenye mazungumzo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako