• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China haitaki kufanya vita wala kuanzisha vita vya biashara

  (GMT+08:00) 2018-03-11 17:29:54

  Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan amesema, hakuna upande unaoshinda kwenye vita vya biashara, na kwamba China haitaki kushiriki kwenye vita vya biashara wala kuanzisha vita hivyo, lakini China inaweza kukabiliana na changamoto yoyote na kulinda kithabiti maslahi ya taifa na wananchi.

  Bw. Zhong amesema hayo alipokutana na wanahabari wa mkutano wa kwanza wa bunge la 13 la umma la China, ambao walitaka kujua kama China na Marekani zitafanya vita vya biashara. Bw. Zhong pia amesema, katika miaka 40 iliyopita, thamani ya biashara kati ya China na Marekani imekua kwa mara 232, huku uwekezaji kwa pande hizo mbili ukizidi dola bilioni 230 za kimarekani.

  Takwimu hizo zimethibitisha kuwa nchi hizo mbili zinashirikiana vizuri kiuchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako