• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Ulaya, Marekani zaendelea na mazungumzo kuhusu ushuru wa chuma na alumini

  (GMT+08:00) 2018-03-12 09:15:30

  Kamishna wa kamati ya Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya biashara Bibi Cecilia Malmstrom, amesema Umoja wa Ulaya na Marekani zitaendelea kufanya mazungumzo kuhusu ushuru wa bidhaa za chuma cha pua na alumini.

  Bibi Cecilia Malmstrom amekutana na mwakilishi wa biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer, ambapo wamejadili kuhusu kufuta ushuru wa bidhaa za chuma cha pua na alumini za Umoja wa Ulaya zinazouzwa nchini Marekani.

  Baada ya mazungumzo hayo, Bibi Malmstrom amesema mchakato halisi wa kusamehe ushuru huo bado haujulikani, lakini wataendelea na mazungumzo wiki hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako