• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNHCR yatahadharisha kuhusu kufanya uamuzi mgumu kutokana na upungufu wa fedha

  (GMT+08:00) 2018-03-12 09:58:47

  Shirika la Umoja wa mataifa la kutoa misaada kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA limetahadharisha kuwa huenda litalazimika kufanya uamuzi mgumu kutokana na upungufu mkubwa wa fedha za bajeti yake.

  Mkurugenzi wa shirika hilo anayeshughulikia operesheni huko Gaza Bw. Matthias Schemale amesema kama nchi wahisani hazitatoa mchango zaidi wa kifedha kwa ajili ya misaada ya afya na elimu kabla ya mwezi Mei, huduma zake zitakabiliwa na hatari.

  Amesema shirika hilo halijafunga taasisi yake yoyote na haijachukua hatua yoyote ya kufanya hivyo, lakini kama nchi hizo wahisani hazitatoa misaada ya fedha kusaidia kazi zake, shirika hilo litafanya maamuzi magumu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako