• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Algeria kuandaa mkutano wa kupambana na ugaidi barani Afrika

  (GMT+08:00) 2018-03-12 16:22:09
   

  Waziri wa mambo ya nje wa Algeria Bw. Abdul Qader al-Masahel amesema, Algeria itaandaa mkutano wa ngazi ya juu wa kupambana na ugaidi barani Afrika mwezi Aprili.

  Bw. Masahel amesema hayo baada ya kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat ambaye yuko ziarani Algeria. Ameongeza kuwa lengo la mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano wa kupambana na ugaidi kati ya nchi za Afrika.

  Bw. Masahel amesema, katika kipindi cha mkutano huo, nchi wanachama wa Umoja wa Afrika watajadili masuala mbalimbali ikiwemo utungaji wa sheria kuhusu ushirikiano wa kupambana na ugaidi, pia zitafikia maoni ya pamoja kuhusu umuhimu wa Umoja wa Afrika kwenye kupambana na ugaidi, kupinga utakatishaji wa fedha, na kupinga biashara haramu ya dawa za kulevya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako