• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Korea Kusini asema mabadiliko ya kasi yatakuja kutokana na mikutano kati ya nchi hiyo, Korea Kaskazini na Marekani

  (GMT+08:00) 2018-03-12 17:48:12

  Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amesema, mabadiliko ya kasi yatakuja kutokana na mikutano kati ya nchi yake na Korea Kaskazini na kati ya Korea Kaskazini na Marekani, ambayo yatafanyika kwa mfululizo katika miezi miwili ijayo.

  Rais Moon amesema hayo katika mkutano wake wa kila wiki na makatibu wake wa ngazi ya juu uliofanyika leo. Amesema fursa muhimu ilianzishwa ili kuweka mazingira ya kuwa na Peninsula ya Korea isiyo na nyuklia, utawala wenye amani ya kudumu na ustawi wa pamoja wa nchi mbili za Korea.

  Kauli ya rais Moon imekuja baada ya nchi mbili za Korea kukubali kufanya mkutano wa marais mwishoni mwa mwezi ujao katika kijiji cha makubaliano ya kusitisha mapigano cha Panmunjom.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako