• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mswada wa marekebisho ya katiba ya China umeonesha kuwa mfumo wa siasa wa China unaendana na wakati

  (GMT+08:00) 2018-03-12 17:49:54

  Mratibu wa ofisi ya Shirika la Global Reporting Initiative barani Afrika Bibi Wadeisor Rukato amesema Bunge la Umma la China kupitisha muswada wa marekebisho ya katiba kumeonesha kuwa mfumo wa siasa wa China unaendana na wakati na una ubora wa kipekee.

  Bi. Rukato kutoka Zimbabwe amesema, ukuaji wa kasi wa China, na hasa mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya uchumi umetoa uzoefu muhimu kwa nchi nyingine. Ongezeko la kasi la uchumi wa China limekuwa chachu kwa nchi zenye mapato ya chini, ambazo zimejifunza uzoefu wa China na kutunga sera husika za maendeleo.

  Pia amesema, hivi sasa China inakabiliwa na changamoto nyingi, likiwemo suala la umaskini, pengo kati ya maendeleo ya miji na vijiji, na uchafuzi wa mazingira, lakini ana imani kuwa China itaendelea kuzidisha nguvu ya mageuzi na kutatua masuala hayo kwenye mchakato wa maendeleo.

  Mkutano wa 13 wa Bunge la Umma la China unaoendelea hapa Beijing, umepitisha muswada wa marekebisho ya katiba, ikiwa ni mara ya kwanza katika miaka 14 iliyopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako