• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Wafanyabiadhara wa Rwanda wasifu huduma za bandari ya Dar es salaam

  (GMT+08:00) 2018-03-12 19:22:45

  Wafanyabiashara wa Rwanda wanaonunua bidhaa kutoka nje wamesifu bandari ya Dar es salaam nchini Tanzania kwa kufungua ofisi mjini Kigali ili kurahisisha upakuaji wa bidhaa zao.

  Sasa kufuatia kufunguliwa kwa ofisi hiyo, wafanyabiashara hawatahitaji tena kusafiri hadi mjini Dar es Salaam kupokea mizigo yao.

  Ofisi hiyo itashughulikia malipo husika na mchakato mzima wa kupakua bidhaa na hivyo kuwapunguzia gharama wafanyabiashara hao.

  Bandari ya Dar es Salaam ndio muhimu zaidi kwa upokeaji wa bidhaa za Rwanda ikiwa inashughulikia asilimia 80 ya biashara zake za kimataifa.

  Waziri wa kazi, uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania Profesa Makame Mbarwa, amesema Rwanda ndio mteja wa tatu mkuu wa bandari ya Dar na hivyo ndio sababu wako kenye mchakato wa kuboresha huduma kwao na kuondoa vikwazo vyote.

  Hivi karibuni, Rwanda na Tanzania zilikubaliana kujenga reli ya wastani ya kilomiyta 521 kutoka Isakakwenda Kigali kwa gharama ya zaidi ya dola bilioni $2.5.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako