• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda yaeleza wasiwasi juu ya kupoteza mali zake Kenya

    (GMT+08:00) 2018-03-12 19:23:46

    Uganda inafanya mazungumzo na Kenya juu ya kukodisha nyumba zake katika eneo la Mombasa huku serikali ya Kenya ikianza kutekeleza sheria mpya ya ardhi ambayo inakataza wageni kumiliki mali karibu na mipaka.

    Ripoti ya ukaguzi inasema Uganda inaweza kupoteza mali inayomilikiwa na serikali yake huko Mombasa,

    Mali hizo ni pamoja na vyumba vya kibiashara vilivyomilikiwa na Uganda chini ya Wizara ya Mambo ya Nje.

    Katika ripoti yake ya ukaguzi kwa Bunge, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, nchini Uganda John Muwanga, alisema sheria mpya itaathiri moja kwa moja mali hizo.

    Hata hivyo waziri wa Mahusiano ya Kimataifa wa Uganda Henry Okello Oryem, , alisema serikali inazungumza na Kenya juu ya utekelezaji wa sheria hiyo ya ardhi.

    Lakini naye Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Ardhi,wa Kenya Muhammad Swazuri, ameondoa hofu kwamba Uganda inaweza kupoteza mali hiyo, ikisema, ikiwawataomba upya ukondishaji wao wataruhusiwa kuendelea kumiliki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako